SHUJAA WA MAENDELEO NA USTAWI WA JAMII
TANZANIA

HEKIMA NA UMOJA, USHINDI NA USHUJAA SMAUJATA

Kuhusu sisi

SMAUJATA ni jumuiya ya kijamii ambayo imesajiliwa chini ya sheria ya asasi za kiraia (CAP .337 RE 2022) kwa usajili namba S.A.23969, SMAUJATA ilianzishwa na shujaa Sospeter Mosewe Bulugu mwaka 2022 kwa lengo la kuchochea mabadiliko chanya na kuleta   maendeleo endelevu kijamii na kiuchumi.

Dira yetu

Dira ya SMAUJATA ni kuwa na Taifa lenye kizazi huru chenye Haki na Usawa Kitakachoweza Kujitegemea na Kuzitambua na kutumia Ujuzi, Maarifa na Vipaji katika kujenga jamii yenye Maendeleo Endelevu

Dhamira yetu

Dhamira Ya SMAUJATA ni Kuiwezesha na Kuijengea Jamii uwezo wa kutambua na kuiishi Misingi ya Haki na Usawa ili kutumia ujuzi, maarifa na vipaji katika kujenga jamii yenye Maendeleo Endelevu.

Imani Yetu Mashujaa

Imani ya SMAUJATA ni “HEKIMA NA UMOJA“, “USHINDI NA USHUJAA SMAUJATA“

Malengo Ya SMAUJATA

Dhana Ya Jumuiya Ya SMAUJATA

Dhana ya Jumuiya ya SMAUJATA ipo katika kupinga vikali, Kuibua na Kutokomeza aina zote za matukio au vitendo vya ukatili katika makundi mbali mbali ya jamii kupitia wananchi wazalendo na wadau mbali mbali kushiriki moja kwa moja katika maeneo yao dhidi ya vitendo hivi viovu

Kauli mbiu ya jumuiya hii imelenga kuhamasisha wananchi kila mmoja kushiriki kufanya yafuatayo:-

  1. KUELIMIKA na kuelimisha wengine kuhusiana na masuala yanayohusu ukatili ikiwa pamoja na kufahamu aina za ukatili madhara yake, hatua za kuchukua dhidi ya vitendo hivi na kufahamu ushiriki wa wananchi katika hili.
  2. KUWA MUANGALIZI WA JAMII na kuchukua hatua kwa kupaza sauti dhidi ya vitendo vya ukatili.
  3. KUSHAURI asas, wadau wa maendeleo, jamii, serikali na vyombo mbali mbali vya maamuzi katika kufanya maboresho mbali mbali ya huduma za kijamii hasa zile ambazo zikiwa hafifu zinaweza kuchochea vitendo vya kikatili

Fahamu Zaidi Kuhusu SMAUJATA

SMAUJATA ilizinduliwa rasmi mnamo Juni 16, 2022 na Mh Dorothy Gwajima (Mb) – Waziri Wa Maendeleo Ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Katika maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika yaliyofanyika kitaifa Jijini Dodoma.

SMAUJATA ni kifupi cha maneno Shujaa Wa Maendeleo na Ustawi wa Jamii Tanzania.

SMAUJATA inaendesha kampeni huru ya kitaifa ya wananchi wazalendo wanao jitolea kuibua, kupambana na kutokomeza vitendo vya ukatili ambapo kufikia Septemba 2024 Jumla ya Watanzania 10,675 katika Mikoa yote nchini wamejiunga na Jumuiya hii.

UONGOZI WA SMAUJATA

Shujaa Sospeter Mosewe Bulugu

Mwasisi na Kiongozi Mkuu wa Jumuiya

Scroll to Top